Monday, February 2, 2015

AFCON 2015: BAADA YA ALGERIA KUNG'OKA, IVORY COAST SASA KUKWAANA DRC.

IVORY Coast jana walifanikiwa kuwang’oa vigogo wenzao Algeria na kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon. Mabao yaliyofungwa na mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester City Wilfried Bony katika dakika ya 26 na 68 na lile lililofungwa na Gervinho katika dakika ya 90 yalitosha kuihakikishia ushindi wa mabao 3-1 waliohitaji Ivory Coast. Sasa Ivory Coast watakwaana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC ambao walitinga hatua hiyo kwa kishindo baada ya kutoka nyuma kwa mabao mawili na kuwafunga majirani zao Congo Brazaville kwa mabao 4-3. Katika mchezo wa robo fainali iliyochezwa awali jana Ghana iliirarua bila huruma Guinea kwa mabao 3-0 ambayo mawili yalifungwa na Cristian Atsu na moja la Kwesi Appiah hivyo kujihakikishia nafasi ya kucheza na wenyeji Guinea ya Ikweta katika hatua ya nusu fainali Ahamisi hii.

No comments:

Post a Comment