Wednesday, February 11, 2015

BAADA YA LIGI KUU KUVUNA MABILIONI KWA KUUZA HAKI ZA MATANGAZO, WANASIASA UINGEREZA WATAKA FEDHA ZAIDI KUTUMIKA KUIBUA VIPAJI KATIKA NGAZI ZA CHINI.

WANASIASA nchini Uingereza wametaka Ligi Kuu kuwekeza zaidi katika soka la vijana kwenye paundi bilioni 5.14 walizopata kwa kuuza haki za matangazo ya soka la luninga. Kampuni ya michezo ya Sky na BT zilikubali kutoa kitita hicho kilichovunja rekodi kwa ajili ya matangazo ya moja kwa moja ya mpira kwa misimu mitatu kuanzia mwaka 2016-2017, ikiwa ni ongezeko la asilimia 70 kulinganisha na mkataba wa sasa wa paundi bilioni tatu. Waziri kivuli wa michezo wa chama cha Labour, Clive Efford amesema itakuwa sio vibaya kama fedha zaidi haziwekezwa katika ngazi za chini za soka. Kauli huyo inaungwa mkono na waziri wa michezo wan chi hiyo Helen Grant ambaye anaielezea Ligi Kuu kama yenye mafanikio zaidi katika historia ya Uingereza huku akiunga mkono kuwekezwa kwa fedha zaidi katika ngazi za chini ili kudumisha na kuboresha historia hiyo ya kipekee. Nao wadau na wachambuzi mbalimbali wa soka nchini humo wameitaka Ligi Kuu kuangalia uwezekano wa kupunguza beki za tiketi ili kila aweze kuudu kwenda uwanjani kutokana na dili hilo kubwa la fedha walilopata. Nyota wa zamani wa kimataifa wa Uingereza, gary Lineker na Jamie Carragher wamedai moja ya mipango ya kuongeza mapato ya mlangoni ni kupunguza bei za tiketi ili mashabiki wengi zaidi waweze kuhudhuria viwnajani kushuhudia timu zao.

No comments:

Post a Comment