Wednesday, February 11, 2015

RAIS WA IVORY COAST AMWAGA MAMILIONI YA EURO KAMA BAKSHISHI KWA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA KWA KUNYAKUWA TAJI LA AFCON.

RAIS wa Ivory Coast Alassane Ouattara amemwaga bakshishi ya euro milioni tatu kuwatunza wachezaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo ambao wamefanikiwa kunyakuwa taji la Mataifa ya Afrika mwaka huu. Ivory Coast ilifanikiwa kuwachapa Ghana kwa changamoto ya mikwaju ya penati 9-8 Jumapili iliyopita katika mchezo wa fainali na kufanikiwa kushinda taji lao la pili la michuano hiyo baada ya lile la mwaka 1992. Kocha wa timu hiyo Herve Renard alialikwa katika ikulu ya rais huyo jana na kupewa bakshishi ya euro milioni 114,000. Waziri wa michezo wan chi hiyo, Alain Lobognon amedai kuwa kila mchezaji katika kikosi cha wachezaji 23 wa timu hiyo amepewa nyumba yenye thamani ya euro 46,000 pamoja na kiasi cha kama hicho cha fedha taslimu. Shirikisho la Soka la Ivory Coast limepewa euro 380,000, huku benchi la ufundi wenyewe wakigawana euro 460,000, hivyo kufanya jumla ya fedha zilizotolewa na rais kufikia euro milioni tatu. Kikosi kizima cha timu hiyo pia kimetunukiwa tuzo za heshima wakitambulika kama mashujaa wan chi hiyo.

No comments:

Post a Comment