MSHAMBULIAJI mkongwe wa kimataifa wa Australia Tim Cahill ametangaza kuwa anatarajia kujiunga na klabu ya Shanghai Shenhua ya China baada ya kutengua mkataba wake na klabu ya New York Red Bulls ya Marekani. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 35 ambaye alikuwemo katika kikosi cha timu ya taifa ya Australia kilichonyakuwa Kombe la Asia mwishoni mwa wiki iliyopita alithibitisha taarifa hizo baada ya kufanya mazungumzo na klabu kadhaa kubwa. Cahill amesema kabla ya kufikia uamuzi huo aliomba ushauri kwa meneja wake wa zamani alipokuwa Everton David Moyes, mchezaji mwenzake wa zamani wa Red Bull Thierry Henry na kocha wa Australia Ange Postecoglou. Nyota huyo amesema amepata ushauri mzuri kutoka kwa watu wenye nguvu sana na kuona huo ndio uamuzi sahihi aliochukua. nCahill amesema uamuzi huo hausiani na masuala ya fedha kwani ingekuwa hivyo angeweza kwenda Qatar au China kabla ya kuitumikia Red Bulls.
No comments:
Post a Comment