MSHAMBULIAJI mkongwe Samuel Eto’o anatarajiwa kuendelea kubakia katika klabu ya Sampdoria pamoja na taarifa kuwa alikwepa kufanya mazoezi ya ziada aliyopewa na kocha Sinisa Mihajlovic. Kocha huyo raia wa Serbia alimtuhumu Eto’o kwa kukosa heshima kwa kukosa mazoezi hayo ya jana. Chanzo cha ndani kilicho karibu na mshambuliaji huyo aliyejiunga na Sampdoria akitokea Everton Jumanne iliyopita kimedai kuwa hakuna ukweli wowote kuhusiana na taarifa za kutaka kuondoka kwa nyota huyo. Chanzo hicho pia kiliendelea kudai kuwa Eto’o mwenye umri wa miaka 33 hawezi kuondoka kwasababu tayari ameshacheza katika vilabu viwili msimu huu na hawezi kuruhusiwa kucheza zaidi ya hapo. Kocha huyo alitaka wachezaji wa kikosi chake kufanya mazoezi ya ziada jana baada ya kipigo cha mabao 5-1 walichpata kutoka kwa Torino Jumapili iliyopita.
No comments:
Post a Comment