MJUMBE wa bodi ya Chama cha Soka cha Misri-EFA, Mahmoud Al Shamy amebainisha kuwa wako tayari kukubaliana na masharti yote ya Mfaransa Herve Renard ili aweze kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo. El Shamy amesema EFA ilitangaza Jumamosi iliyopita kuwa imeshafikia maamuzi katika orodha ya makocha watano na wanatarajia kutangaza jina la kocha mpya wiki hii. Mjumbe huyo aliendelea kudai kuwa walikuwa na majina matano lakini walifanya mazungumzo na makocha watatu pekee. El Shamy amesema wamezungumza na Renard, Alain Giresse na George Leekens na mapema wanatarajiwa kutangaza jina la kocha wao mpya.
No comments:
Post a Comment