MENEJA wa klabu ya Manchester United, Louis van Gaal amesema anatarajia kuongeza mchezaji wa nafasi ya kiungo katika usajili wa majira ya kiangazi. Van Gaal amekuwa akikosolewa kwa kumchezesha mshambuliaji Wayne rooney katika nafasi ya kiungo na alipoulizwa kama atahitajika kusaini kiungo mpya akakubali. Kocha huyo amesema kwasasa anaangalia uwiano katika nafasi ya kiungo hususani kutokana na wachezaji alionao katika nafasi hiyo kama Adnan Januzaj na Angel Di Maria. Van Gaal aliendelea kudai kuwa Rooney mwenye umri wa miaka 29 ambaye hajafunga bao katika mechi tisa zzilizopita, hana tatizo na kucheza katika nafasi ya kiungo kwani hajawahi kumfuata na kumueleza chochote. United wanakabiliwa na mchezo wa Kombe la FA leo dhidi ya Preston.
No comments:
Post a Comment