NAHODHA wa kikosi cha timu ya taifa ya Ghana, Asamoah Gyan amedai hatomsamehe golikipa wa Guinea Naby Yattara kutokana na faulo aliyomchezea katika mchezo wa Mataifa ya Afrika uliokutanisha timu hizo. Golikipa huyo alimkanyaga Gyan kwa teke la tumboni katika dakika za mwisho za mchezo wa robo fainali uliokutanisha timu hizo. Yattara alilimwa kadi nyekundu lakini hajapewa adhabu yeyote nyingine mpaka sasa. Akihojiwa Gyan amesema bado analitaka Shirikisho la Soka la Afrika-CAF kumtwanga adhabu Yattara kwasababu anadhani alidhamiria kufanya tukio lile. Gyan aliendelea kudai kuwa ilikuwa ni faulo mbaya ambayo ingeweza kumsababisha asicheze tena soka ndio maana hataki kumsamehe kwa hilo.
No comments:
Post a Comment