Sunday, February 8, 2015

MAN UNITED YALITAKA BEKI LA FEYENOORD KIANGAZI.

KLABU ya Manchester United inaongoza mbio za kumuwania beki chipukizi wa klabu ya Feyenoord Terence Kongolo katika majira ya kiangazi. Kongolo yuko katika rada za kocha wa zamani wa Feyenoord Ronald Koeman kwenda Southampton wakati Manchester City nao wameonyesha nia ya kumuunganisha nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 na kaka yake Rodney ambaye anacheza katika kikosi chao cha vijana chini ya umri wa miaka 18. Hata hivyo, United ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kumsajili Kongolo huku Louis van Gaal akitajwa kumhusudu beki huyo wa kati kwa kumpa nafasi ya kuitumikia timu ya taifa ya Uholanzi kwa mara ya kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana. Van Gaal atakuwa sokoni kutafuta mabeki katika majira ya kiangazi na atakuwa akiangalia kusajili mabeki wenye ubora kama Mats Hummels au Diego Godin.

No comments:

Post a Comment