MSHAMBULIAJI wa Newcastle United, Siem de Jong anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki nane kutokana na matatizo ya mapafu. Nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 26 ambae alisajiliwa kutoka Ajax Amsterdam majira ya kiangazi mwaka jana anatarajiwa kufanyiwa upasuaji kesho. De Jong alipata tatizo kama hilo mwaka 2013 lakini alipona kurejea uwanjani kabla ya tatizo hilo kumrudia tena. Nyota huyo ambaye alikuwa tayari ameanza mazoezi ya kurejea katika kikosi cha kwanza baada ya kusumbuliwa na majeruhi katika siku za karibuni, amesema amesikitishwa kwa kurudi tena nyuma baada ya juhudi kubwa alizofanya. De Jong amesema kwa miezi kadhaa amekuwa akifanya bidii ili aweze kuwa fiti kwa asilimia mia moja hivyo anajiona kama ana bahati mbaya kupata tatizo lingine ambalo litamrudisha nyuma.
No comments:
Post a Comment