SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF limepanga kutuma maombi ya mabadiliko ya sheria ambayo itamruhusu Issa Hayatou kuongeza kipindi kingine katika uongozi wake. Hayatou raia wa Cameroon alichaguliwa kuongoza CAF miaka 27 iliyopita na baadhi ya maofisa ambao wamekuwa kugombea nae wamekuwa wakishindwa vibaya katika sanduku la kura. Lakini kwa mujibu wa sheria za CAF, inazuia kiongozi kuongoza akiwa na umri zaidi ya miaka 70 jambo ambalo linamzuia Hayatou ambaye sasa ana umri wa miaka 68 huku akitaka kugombea kwa kipindi cha nane mwaka 2017. Mjumbe mmoja wa kamati ya utendaji ya CAF kutoka Ghana Kwesi Nyantakyi aliwaambia wanahabari jijini Malabo kuwa shirikisho hilo limepanga kufuata njia inayotumiwa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA ya kutokuwa na kikomo cha umri kwa viongozi wake. Nyantakyi amesema FIFA hawana kikomo cha umri kwa wajumbe wake wa kamati ya utendaji hivyo CAF nao wanataka wafanye kama hivyo kwa wajumbe wake.
No comments:
Post a Comment