Wednesday, February 11, 2015

MPANGO WA MADRID KUENDELEZA UWANJA WA SANTIAGO BERNABEU WAKWAMA.

MPANGO wa Real Madrid kutumia mamilioni ya euro kwa ajili ya kuendeleza Uwanja wa Santiago Bernabeu umekwama baada ya makubaliano na baraza la mji huo kuzuiwa na mahakama. Mabingwa hao wa Ulaya walikuwa na mpango wa kuuboresha uwanja huo lakini Mahakama Kuu ya Madrid imetoa zuio la muda kufuatia uchunguzi unaoendelea kuhusiana na suala la ardhi. Kwa mujibu mahakama kumekuwa na malalamiko kuhusu uboreshaji huo na jamii ambayo itaathirika kwa ardhi yao kuchukuliwa na kuhamishwa katika eneo la mradi. Kufuatia hali hiyo klabu hiyo sasa italazimika kufanya kazi na baraza la jiji na jamii inayozunguka eneo hilo kuelezea nia yao na kutoa malipo stahidi kwa waathirika ili ujenzi huo uweze kufanyika bila vikwazo. Real Madrid ilitangaza mpango wake huo wa uboreshaji ambao ungegharimu kiasi cha euro milioni 400 na kuufanya uwanja huo kuwa moja ya viwanja bora kabisa duniani ambao ungejumuisha sehemu za burudani, migahawa, hoteli na eneo la maegesho la chini ya ardhi.

No comments:

Post a Comment