MENEJA wa msaidizi wa Liverpool, Colin Pascoe amesema bao la kwanza la Ligi Kuu lililokuwa likisubiriwa na Mario Balotelli linaweza kuwa mwanzo wa mvua ya mabao kwa nyota huyo. Balotelli alitokea benchi na kuifungiwa timu yake bao la ushindi katika dakika ya 83 na kuipa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Tottenham Hotspurs hivyo kufufua matumaini yao ya kumaliza katika nafasi nne za juu katika Ligi Kuu. Hilo linakuwa bao lake la kwanza kwa nyota huyo wa kimataifa wa Italia katika mechi 13 alizoichezea Liverpool na bao lake la kwanza katika Ligi Kuu toka alipofunga wakati akiwa Machester City mwaka 2012. Akihojiwa Pascoe amesema ana matumaini bao hilo la Balotelli ndio utakuwa mwanzo wa nyota huo kufunga mabao mengi zaidi kwani amekuwa akifanya juhudi kubwa. Liverpool wako katika nafasi ya saba katika msimamo wa ligi wakiwa nyuma ya Spurs waliopo nafasi ya sita.
No comments:
Post a Comment