KOCHA wa timu ya taifa ya Nigeria aliyemaliza muda wake Stephen Keshi anakaribia kuteuliwa kuinoa timu ya taifa ya Burkina Faso. Keshi ametajwa katika orodha ya makocha watatu wa mwisho ambao watafanyiwa usaili kwa ajili ya kibarua hicho. Shirikisho la Soka la Burkina Faso-FBF jana kilitaja majina hayo ambapo mbali na Keshi lakini pia inawajumuisha Milovan Rajevac kutoka Serbia na Gernot Rohr wa ujerumani. Baada ya kuwafanyia usaili FBF inatarajia kutangaza jina la kocha atakaechukua nafasi ya Paul Put katika kipindi cha wiki tatu zijazo.
No comments:
Post a Comment