MENEJA wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini amekataa kulaumu kukosekana kwa Yaya Toure kuwa ndio chanzo cha kuporomoka kwa kikosi chake mwaka huu kufuatia sare ya bao 1-1 nyumbani waliyopata dhidi ya Hull City jana. Mabingwa hao watetezi wa ligi Kuu sasa wako nyuma ya vinara Chelsea kwa alama saba huku wakiwa wamecheza mechi nne za ligi bila kupata ushindi. Mbali na hilo City pia walijikuta waking’olewa katika michuano ya Kombe la FA na Middlesbrough inayoshiriki ligi daraja la kwanza. Hayo yote yametokea toka wamkose Toure ambaye amekuwa akiitumikia Ivory Coast katika michuano ya Mataifa ya Afrika. Hata hivyo, akiulizwa kuhusiana na hilo Pellegrini amesema hana shaka kuhusiana na umuhimu wa Toure katika kikosi chake lakini hilo halimaanishi kuwa akikosekana hawawezi kushindsa mechi zao.
No comments:
Post a Comment