MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho hadhani kama tofauti ya alama saba walionayo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ni faida katika mbio zao za kugombea taji hilo. Chelsea imeitandika Aston Villa kwa mabao 2-1 jana, wakati Manchester City wanaowafuata katika nafasi ya pili wakitopa sare na Hull City. Akihojiwa Mourinho, amesema ingekuwa nchi nyingine angeweza kuanza kushangilia katika kwa Uingereza tofauti ya alama saba sio chochote. Mourinho aliendelea kudai kuwa bado kuna mechi 14 na alama 42 za kupigania hivyo kila mchezo unakuwa mgumu na chochpote kinaweza kutokea. Kocha huyo pia alisisitiza hakushtushwa kuona City wakitoa sare nyumbani na Hull ambao wako msatari wa kushuka daraja lakini amefurahi kuona matumaini ya kunyakuwa taji yakiwa mikononi mwao.
No comments:
Post a Comment