RAIS wa Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA Sepp Blatter ameponda vyombo vya habari kuonyesha vurugu zilizozuka katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika kati ya wenyeji Guinea ya Ikweta na Ghana. Mchezo huo uliochezwa Malabo ulisimamishwa kwa dakika 30 baada ya mashabiki kurusha vitu kwa wachezaji na mashabiki wa timu pinzani hali iliyosababisha polisi kutumia helikopta na mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki hao. Vurugu hizo zilikuwa zikirushwa moja kwa moja duniani kote, lakini Blatter anadhani pamoja na vurugu hizo lakini kuna mazuri mengi ya kusifiwa katika michuano hiyo inayotarajiwa kumalizka leo. Blatter amesema siku zote habari nzuri huwa sio habari ila habari mbaya ndio habari akimaanisha kuwa siku zote watu wamekuwa wakizungumzia mabaya. Rais huyo amesema dosari ndogo kama iliyotokea katika mchezo wa nusu fainali haipaswi kupewa nafasi ya kusahau mafanikio yaliyopata katika michuano hiyo ambayo imendaliwa kwa kipindi kifupi kuliko ilivyopangwa.
No comments:
Post a Comment