ULINZI zaidi utaongezwa katika mchezo wa fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika leo kati ya Ivory Coast na Ghana baada ya vurugu za mashabiki zilizotokea katika mchezo nusu fainali Alhamisi iliyopita. Katika mchezo huo ambao Ghana iliwatandika wenyeji Guinea ya Ikweta kwa mabao 3-0 ulisimamishwa kwa zaidi ya dakika 30 kutokana na mashabiki wa nyumbani kurusha chupa za maji uwanjani. Katika mkuu wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF Hicham El Amrani amesema wamepanga utaratibu mpya na watu usalama ili kuhakikisha yaliyotokea nyuma hayajirudii katika mchezo wa fainali. Al Amrani aliendelea kudai kuwa wameongeza watu wengi zaidi wa usalama huku rais wa nchi hiyo naye akiwasihi wananchi wake kwenda kushangilia kwa amani mafanikio waliyopapata katika maandalizi ya michuano hiyo. Fainali ya leo itakuwa kama marudioa ya fainali iliyofanya ya michuano hiyo iliyofanyika mwaka 1992 na kuzikutanisha timu hizo ambapo Ivory Coast walishinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati.
No comments:
Post a Comment