RAIS wa klabu ya Palermo, Mauro Zamparini amesisitiza kuwa afadhali amuuze Paulo Dybala kwa Juventus kuliko Manchester United au klabu yeyote nje ya Italia. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina amekuwa akizivutia baadhi ya klabu kubwa Ulaya kutokana na kiwango bora alichoonyesha msimu huu na Juventus na United zimekuwa zikimfuatilia kwa karibu nyota huyo mwenye umri wa miaka 21. Hata hivyo, Zamparini ambaye uhusiano wake na mchezaji huyo sio wa kuridhisha, amedai angependelea zaidi kama Dybala angebakia Serie A. Hata hivyo, rais huyo amesema kama fungu litakuwa kubwa kwa vilabu vilivyo nje ya Italia atakuwa hana jinsi bali kumuachia aondoke. Zamparini amesema hakuna mawasiliano yeyote na Napoli lakini Juventus tayari wameshafanya mawasiliano nao wakitaka kumsajili mchezaji huyo. Dybala ambaye amefunga mabao 11 katika mechi 21 za Serie A alizocheza msimu huu, mkataba wake na Palermo unamalizika Juni mwakani.
No comments:
Post a Comment