BABA wa golikipa mahiri wa kimataifa wa Costa Rica, Keylor Navas amesisitiza nyota huyo hana mpango wowote wa kuondoka Real Madrid kwasasa na amepania kupigania nafasi yake katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Navas mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na Madrid akitokea Levante baada ya kuonyesha kiwango bora katika msimu wa 2013-2014 na Kombe la Dunia lakini mpaka sasa ameshindwa kabisa kumnyang’anya namba Iker Casillas kama golikipa namba moja wa Madrid. Lakini pamoja na kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, Navas amegoma kukata tamaa na ataendelea kubakia hapo ili aweze kumshawishi kocha Carlo Ancelotti kumchezesha. Baba wa mchezaji huyo Freddy Navas amesema mwanae huyo alimwambia kuwa hana mpango wa kuondoka Madrid kwani anafurahia kuwepo hapo na atapigana kadri awezavyo kuhakikisha anapata namba mbele ya Casillas.
No comments:
Post a Comment