KLABU ya Bastia ya Ufaransa imetozwa faini ya euro 35,000 leo baada ya mashabiki wake kuonyesha mapango ya kuipinga Qatar wakati wa mchezo wao dhidi ya Paris Saint-Germain-PSG. Bango hilo ambalo lilionyeshwa katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Corsicans Furiani Januari 10 mwaka huu lilikuwa na maandishi yaliyosomeka kuwa Qatar inaidhamini PSG pamoja na ugaidi. PSG inamilikiwa na kampuni ya uwekezaji ya michezo ya Qatar wakiwa wanamiliki hisa asilimia moja. Qatar ni mojawapo iliounda umoja na Marekani kupinga kikundi cha kigaidi cha Dola la Kiislamu lakini wamekuwa wakituhumiwa kuruhusu mirija ya hela kukifikia kikundi hicho jambo ambalo wamelikanusha.
No comments:
Post a Comment