BEKI wa klabu ya Real Madrid, Fabio Coentrao anategemewa kukaa nje ya uwanja mpaka Machi mwaka huu baada ya kupata majeruhi akiwa mazoezini wiki hii. Mabingwa hao wa Ulaya walithibitisha taarifa hizo jana huku wakitegemea nyota huyo kukaa nje akijiuguza kwa kipindi cha wiki tatu. Coentrao ameanza kucheza katika kikosi cha Madrid katika mechi tatu pekee msimu huu huku mbili kati ya hizo ikiwa kipigo cha mabao 4-0 walichopata kutoka Atletico Madrid mwishoni mwa wiki iliyopita. Hata hivyo, kukosekana kwa Coentrao kunamfanya kocha Carlo Ancelotti kupata upungufu katka safu yake ya ulinzi wakati huu ambapo mechi za mtoano za Ligi ya Mabingwa Ulaya zikikaribia kuanza.
No comments:
Post a Comment