Friday, February 13, 2015

BARCELONA YAMCHUKUA MKURUGENZI WA ZAMANI WA MICHEZO WA AC MILAN.

KLABU ya Barcelona imemteua mkurugenzi wa zamani wa michezo wa klabu ya AC Milan Ariedo Braida katka kamati mpya ya ufundi ili kusaidia mipango katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Braida ambaye alifanya kazi Milan kuanzia mwaka 1986 mpaka 2013, ataungana na mchezaji wa zamani wa Barceona na kocha Carles Rexach, makamu wa raia Jordi Mestre na mkurugenzi wa klabu hiyo Javier Bordas katika kamati hiyo. Klabu hiyo imemua kuunda bodi mpya mbayo itafanya kazi kwa karibu zaidi na kocha Luis Enrique, kufuatia kutimuliwa kwa aliyekuwa mkurugenzi wa michezo Andoni Zubizarreta mwezi uliopita. Rekodi ya Zubizarretta katika soko la usajili haikuwa ya kuridhisha na alikuwa akilaumiwa kwa kushindwa kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo msimu uliopita hatua iliyochangia timu hiyo kutonyakuwa taji lolote.

No comments:

Post a Comment