Friday, February 13, 2015

NASRI AMTUHUMU DESCHAMPS KUMNYIMA NAFASI YA KUTIMIZA NDOTO ZAKE.

KIUNGO wa klabu ya Manchester City, Samir Nasri amemtuhumu Didier Deschamps kumnyima nafasi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia na kudai kuwa hawezi kusahau kitendo kamwe. Nyota huyo alikuwa katika kiwango bora msimu wa 2013-2014 akiisaidia City kushinda taji la Ligi Kuu huku akiwa na nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha Manuel Pellegrini. Hata hivyo, Nasri aliachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kilishoshiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana nchini Brazil na Deschamps hivyo kumfanya kuamua kustaafu soka la kimataifa mapema akiwa na umri wa miaka 27. Nasri amesema kukosa kucheza katika Kombe la Dunia ni mambo yalimhuzunisha katika kazi yake ya soka hivyo hawezi kumsamehe kamwe Deschamps kwa kumuacha katika kikosi chake.

No comments:

Post a Comment