MCHEZAJI wa zamani wa Barcelona, Eric Abidal amesema Lionel Messi sio mashine lakini atabakia kuwa mchezaji wa kipekee. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa alicheza kwa kipindi cha miaka sita Camp Nou na nyota huyo wa Argentina kabla ya kutimkia Monaco mwaka 2013. Ingawa ameshindwa kunyakuwa tuzo mbili za Ballon d’Or zilizopita, Messi amekuwa katika kiwango bora toka kuanza kwa mwaka huu na Barcelona imepunguza pengo la alama mpaka kufikia moja nyuma ya vinara wa La Liga Real Madrid wakiwa wameshinda mechi 10 mfululizo. Abidal amesema Messi yuko katika kiwango chake kwa asilimia mia moja jambo ambalo lilikuwa likitegemewa na wengi mwaka huu. Abidal aliendelea kudai kuwa wachezaji wakubwa wataendelea kuwa wakubwa lakini sio mashine na hiyo inakwenda hata kwa Messi lakini akiwa katika kiwango chake cha juu kila kitu kinakwenda sawa kwa Barcelona.
No comments:
Post a Comment