Friday, February 13, 2015

SINA HISTORIA YA KUMUUMIZA MCHEZAJI YEYOTE KWA MAKUSUDI - COSTA.

MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Diego Costa amedai kuwa mchezo wake ni wa kutumia nguvu lakini wa kawaida na hajawahi kumuumiza vibaya mchezaji yeyote wa timu pinzani. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania na mzaliwa na Brazil mwenye umri wa miaka 26, anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu kwa kumkanyaga Emre Can wa Liverpool katika mchezo wao wa nusu fainali ya Kombe la Ligi mwezi uliopita. Akihojiwa Costa amesema huwa anapenda kutumia nguvu akiwa mchezoni lakini kamwe hajawahi kumuumiza mchezaji yeyote vibaya. Meneja wa Chelsea Jose Mourinho naye pia amemtetea Costa na kudai alimkanyaga Can kwa bahati mbaya na sio makusudi kama wengi wanavyodai.

No comments:

Post a Comment