Monday, February 2, 2015

TETESI ZA USAJILI ZILIZOPAMBA VICHWA VYA HABARI KATIKA SIKU YA MWISHO YA USAJILI UINGEREZA: UNITED YAWATAKA KWA PAMOJA BRUYNE NA HUMMELS, STOKE YAMNYEMELEA ADEBAYOR.

WAKATI zikiwa zimebakia saa chache kabla ya dirisha la usajili halijafungwa leo usiku, klabu ya Manchester United imepanga kuwasajili mshambuliaji wa Wolfsburg Kevin Bruyne mwenye umri wa miaka 23 na beki wa Borussia Dortmund Mats Hummels mwenye umri wa miaka 26. Beki wa Manchester City Micah Richards mwenye umri wa miaka 26 ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ay Fiorentina anatarajiwa kukataa ofa za kujiunga na Chelsea na Liverpool na badala atajiunga na Inter Milan ilikuungana na kocha wa zamani wa City Roberto Mancini. Klabu ya Everton inajipanga kukamilisha dili la kumchukua kwa mkopo winga wa Man United Adnan Januzaj mwenye umri wa miaka 19 kutokana na nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji kushindwa kuimarika chini ya kocha Louis van Gaal. Meneja wa Stoke City Mark Hughes anajipanga kutuma ofa katika siku hii ya mwisho ya usajili leo kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Emmanuel Adebayor mwenye umri wa miaka 30 ambaye aliwahi kuwa chini yake wakati akiwa City. Southampton wana matumaini ya kukamilisha dili la paundi milioni tano kwa ajili ya usajili wa kiungo wa Feyenoord Tonny Vilhena mwenye umri wa miaka 20. Newcastle United wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Aston Villa na Tottenham Hotspurs kwa ajili ya kumsajili kiungo wa MK Dons Dele Alli mwenye umri wa miaka 18. Naye Darren Fletcher anaweza kuondoka Man United kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili leo huku West Bromwich Albion wakiwa tayari kumchukua kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31. United nao bado wana matumaini ya kumsajili Marquinhos mwenye umri wa miaka 30 kutoka klabu ya Paris saint-Germain pamoja na mabingwa hao wa Ufaransa kupiga chini ofa ya paundi milioni 35 iliyotolewa na United kwa ajili ya beki huyo wa kimataifa wa Brazi.



0000

No comments:

Post a Comment