MMOJA wa wagombea urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Jerome Champagne amejitoa katika kinyang’anyiro hicho baada ya kushindwa kupata kuungwa mkono vya kutosha. Mgombea huyo raia wa Ufaransa ambaye alikuwa anahitaji kuungwa mkono na mashirikisho kutoka katika nchi tano amesema ameungwa mkono na mashirikisho matatu pekee. Katika taarifa yake Champagne amesema anasikitika kutanga kuwa ameshindwa kupata barua tano za kuungwa mkono na mashirikisho kwa ajili ya kuwa mgombea wa nafasi hiyo. Champagne mwenye umri wa miaka 56 ambaye ni mjumbe wa zamani wa kamati ya utendaji ya FIFA amelilaumu Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA na taasisi zake kuchangia kuondolewa katika nafasi hiyo. Uchaguzi wa FIFA unatarajiwa kufanyika Mei 29 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment