MSHAMBULIAJI wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry amekiri kumwaga machozi wakati akiondoka katika klabu hiyo mwaka 2007 na kubanisha alikuwa akifikiria atakuwa mshambuliaji chaguo la nne katika kikosi cha Barcelona kilichokuwa chini ya Pep Guardiola. Henry ambaye alitangaza kutundika daruga zake Desemba mwaka jana, aliisaidia Arsenal kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu na matatu ya Kombe la FA wakati pia akibakia kuwa mfungaji mwenye mabao mengi zaidi katika klabu hiyo. Akihojiwa Henry amesema hakuwahi kufikiria kuikacha Arsenal lakini alikuwa na umri wa miaka 29 huku akiwa katika kiwango cha juu huku akiwa hana uhakika kama meneja Arsene Wenger angebakia. Henry aliendelea kudai kuwa haikuwa kazi rahisi na wakati akiondoka alilia machozi na haoni haya kulisema hilo kwani ni klabu aliyokuwa akiipenda kutoka moyoni. Baada ya kujiunga na Barcelona kwa kitita cha euro milioni 21.3, Henry amesema ilibidi alazimishe kuingia katika mipango ya Guardiola kwani alishaambiwa atakuwa chaguo la nne katika safu ya ushambuliaji jambo alikubaliana nalo.
No comments:
Post a Comment