KLABU ya AS Roma imepata pigo lingine jana baada ya kuthibitishwa kuwa mshambuliaji wake Juan Manuel Iturbe amepata majeraha ya goti na kifundi cha mguu wakati wa mchezo uliomalizika kwa sare ya baa 1-1 dhidi ya Empoli. Katika taarifa yake, Roma ilithibitisha taarifa hizo katika mtandao wake leo baada ya mchezaji huyo kufanyiwa vipimo. Ingawa Roma hawakueleza kama mchezaji huyo atahitaji upasuaji lakini vyombo vya habari nchini Italia vimedai kuwa nyota huyo atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki sita. Nyota huyo alituma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akithibitisha taarifa hizo na kudai kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha anarejea akiwa imara zaidi. Iturbe ambaye amezaliwa na nchini Argentina na kukulia Paraguay alijiunga na Roma akitokea Verona mwaka jana.
No comments:
Post a Comment