MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anaamini Olivier Giroud amebadilika kama mchezaji katika kipindi alichokuwepo katika timu hiyo, kufuatia mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Middlesbrough. Ushindi huo unaoifanya Arsenal kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo na Wenger ameonyesha kufurahishwa na kiwango cha nyota huyo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Wenger amesema anaamini Giroud amebadilika kulinganisha na alivyotua katika timu hiyo mwaka 2012. Wenger aliendelea kudai kuwa sasa nyota huyo anafahamu kitu gani kinahitajika katika soka la kiwango cha juu.
No comments:
Post a Comment