Monday, February 16, 2015

WESTBROOK AIBUKA NA TUZO YA MVP WAKATI KANDA YA MAGHARIBI IKIIGARAGAZA KANDA YA MASHARIKI KATIKA KIKAPU.

Lebron James akipanga mbinu za kumpita Chris wa kanda wa magharibi katika mchezo huo.
MCHEZAJI nyota wa mpira wa kikapu Russell Westbrook, alfajiri ya kuamkia leo aliiongoza Kanda ya Magharibi kuichapa Kanda ya Mashariki kwa vikapu 163-158 katika mchezo wa ulioshirikisha nyota wote wa NBA ambao umevunja rekodi ya kufungwa alama nyingi zaidi. Westbrook ambaye anacheza katika timu ya Oklamhama City alifunga vikapu 41 ya kunyakuwa tuzo ya Mchezaji Mwenye Thamani Zaidi-MVP huku nyota mwingine Lebron James akifunga vikapu 30 kwa upande wa Kanda ya Mashariki. 
Nyota wa zamani wa mpira wa kikapu rais wa DR Congo, Dikembe Mutombo akiwa na rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton wakifuatilia kwa karibu mchezo huo.
Mchezo huo wa maonyesho huwashirikisha wachezaji nyota kutoka kanda zote wa NBA. Vikosi katika timu za kanda zote huchaguliwa na mashabiki wa mchezo ambapo kwa mwaka huu tumeshuhudia rekodi ikivunjwa kwa kufungwa alama nyingi zaidi kuliko mechi yeyote iliyokutanisha kanda hizo.

No comments:

Post a Comment