WAKALA wa Dani Alves amebainisha kuwa beki huyo wa Barcelona yuko katika mazungumzo na klabu nyingine kwa ajili ya kuondoka katika majira ya kiangazi. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 31, anakaribia kumaliza mkataba wake na Barcelona na bado hajapewa ofa yeyote na timu hiyo. Wakala huyo Dinorah Santana amesema wanakaribia kukamilisha mazungumzo hayo na Alves anaweza kuondoka Barcelona mwishoni mwa msimu. Alves alijiunga na Barcelona akitokea Sevilla katika majira ya kiangazi mwaka 2008 na toka wakati huo amekuwa mchezaji muhimu akisaidia kushinda mataji manne ya La Liga, moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia, Kombe la Mfalme na Super Cup.

No comments:
Post a Comment