Wednesday, March 4, 2015

VAN GAAL AMKINGIA KIFUA DI MARIA.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, Louis van Gaal amesema hajui Angel Di Maria atatumia muda gani kuzoea mazingira ya Ligi Kuu. Baada ya kuanza vyema alipotua Old Trafford, Di Maria ambaye alisajiliwa kwa kitita kilichovunja rekodi cha paundi milioni 59.7 akitokea Real Madrid lakini ameshindwa kuendelea kung’aa hivi karibuni. Akihojiwa Van Gaal, amesema wachezaji wote waliowanunua huwa siku zote wanapata wakati mgumu katika msimu wa kwanza. Van Gaal amesema sio Di Maria pekee anayepigana kuzoea mazingira lakini pia wapo Luke Shaw, Daley Blind, Ander Herrera na Radamel Falcao ambao nao wamekuwa wakipata tabu kuzoea.

No comments:

Post a Comment