RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter amekataa ofa ya pamoja kutoka kwa mashirika ya BBC na Sky kushiriki katika mdahalo wa wagombea urais katika uchaguzi wa shiriki hilo utakaoonyeshwa moja kwa moja. Mahasimu wake watatu katika kiinyang’anyiro hicho wamekubali mualiko huo lakini wote wamesisitiza kuwa mdahalo huo ushirikishe wagombea wote ikiwa ni moja masharti yao. BBC na Sky walikuwa wamepanga kuwashirikisha mashabiki wa soka ambao wangepata nafasi ya kuuliza maswali kwa wagombea. Miongoni mwa wagombea wanaopambana na Blatter katika uchaguzi huo ni pamoja na rais wa Shirikisho la Soka la Jordan Prince Ali Bin Al Hussein, rais wa Shirikisho la Soka la Uholanzi Michael van Praag na winga wa zamani wa kimataifa wa Ureno na klabu za Barcelona, Real Madrid na Inter Milan, Luis Figo. Blatter mwenye umri wa miaka 79, atakuwa akigombea kipindi cha tano toka akwae madaraka kwa mara ya kwanza mwaka 1998.
No comments:
Post a Comment