MFUNGAJI wa bao pekee katika mchezo wa jana kati ya Barcelona na Manchester City, Ivan Rakitic ametania kuwa hata wapinzani wao walikuwa wakifurahia kumuona Lionel Messi anavyocheza. Rakitic alifunga bao hilo katika ushindi wa bao 1-0 waliopata Barcelona uliowavusha katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa jumla ya mabao 3-1. Akihojiwa Rakitic amesema hakuna maneno zaidi mazuri ambayo unaweza kumuelezea Messi kutokana na kiwango bora alichoonyesha katika mchezo wao wa jana. Nyota huyo wa kimataifa wa Croatia aliendelea kudai kuwa anadhani hata wachezaji wa City walifurahia kuona jinsi Messi anavyocheza na anatumaini ataendelea kucheza kwa kiwango hicho. Rakitic pia alimpongeza golikipa wa City Joe Hart kwa juhudi kubwa ya kuzuia michomo yao mingi katika mchezo wa jana kwani yeye ndiye aliyekuwa kikwazo cha kushindwa kupata mabao mengi.
No comments:
Post a Comment