Wednesday, March 11, 2015

CHAMPIONS LEAGUE 2015: MADRID WATINGA ROBO FAINALI KWA MBINDE.

PAMOJA na Real Madrid kuchapwa mabao 4-3 na Schalke ya Ujerumani katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, timu hiyo imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. Madrid imenufanika na matokeo ya mechi ya mkondo wa kwanza ambapo iliwalaza Schalke kwa mabao 2- 0 na hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 5-4. Mshambuliaji nyota wa Madrid, Cristiano Ronaldo alivunja rekodi kwa kuwa mhcezaji pekee aliyefunga mabao mengi zaidi katika michuano hiyo baada ya kufunga mabao mawili na kufikisha jumla ya mabao 78. Awali rekosi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na nguli wa zamani wa Madrid Raul aliyewahi kufunga mabao 77 huku mshambuliaji nyota wa Barcelona Lionel Messi naye akiwa nyuma yao kwa kuwa mabao 76 katika michuano hiyo. Katika mchezo mwingine wa michuano uliochezwa jana FC Porto ya Ureno nayo iilifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuichapa FC Basel kwa mabao 4-0 hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao ya mabao 5-4 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wao wa kwanza.

No comments:

Post a Comment