MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amewaambia waandishi kuwa hatazungumza na vyombo vya habari mpaka mwishoni mwa msimu baada ya kuisaidia timu yake kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alifunga mabao mawili wakati mabingwa hao watetezi walipochapwa mabao 4-3 na Schalke ya Ujerumani. Katika mchezo huo Ronaldo alionyesha wazi kukasirishwa muda wote wa mchezo baada kunaswa katika picha za video akimwambia mchezaji mwenzake Karim Benzema kuwa wanacheza mchezo wa aibu mbele ya mashabiki wao. Mara baada ya mchezo kumaliza Ronaldo alionekana akiondoka haraka uwanjani kabla ya kuitwa na nahodha wake Iker Casillas kwa ajili ya kusalimiana na mashabiki. Akiwa njiani kuelekea katika vyumba vya kubadilishia nguo Ronaldo aliwaambia waandishi wa habari wa eneo hilo kuwa hatazungumza tena na vyombo vya habari mpaka mwishoni mwa msimu.
No comments:
Post a Comment