MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amesema Paris Saint Germain-PSG ni moja timu ngumu kuwahi kukutana nazo msimu huu. Chelsea inatarajiwa kukwaana na PSG baadae leo katika Uwanja wa Old Trafford huku wakimkosa kiungo wake John Mikel Obi ambaye ana majeruhi ya goti. Chelsea ambao katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Paris walitoka sare ya bao 1-1, watakuwa na ahueni baada ya taarifa kuwa Nemanja Matic atakuwepo kufuatia kumaliza adhabu yake aliyokuwa akiitumikia. Mourinho amesema msimu huu wamecheza na timu mbalimbali lakini PSG ndio timu pekee imekuwa ngumu kwao kutokana faulo nyingi wanazocheza. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa kwa ubora wa timu kama PSG alitegemea zaidi soka safi kutoka kwao.
No comments:
Post a Comment