MSHAMBULIAJI wa Newcastle United, Papiss Cisse amekubali mashitaka yaliyotolewa na Chama cha Soka cha Uingereza-FA kwa kumtemea mate beki wa Manchester United Jonny Evans. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29, anaweza kukabiliwa na kifungo cha mechi saba kutokana na tukio hilo ambalo lilitokea wakati wa mchezo ambao United ilishinda bao 1-0 dhidi ya Newcastle Juzi. Evans mwenye umri wa miaka 27 bado hajajibu chochote kuhusiana na mashitaka hayo. Mapema Cisse aliomba radhi kutokana na tukio hilo lakini amekanusha kama alifanya kwa makusudi.
No comments:
Post a Comment