Friday, March 6, 2015

RAIS WA MALI AWAMWAGIA ZAWADI KEDEKEDE VIJANA WA TIMU YA TAIFA YA UNDER17 WALIONYAKUWA TAJI LA AFRIKA.

RAIS wa Mali Ibrahim Boubacar Keita ametoa ofa ya nyumba, kompyuta mpakato au laptop na kusomeshwa bure kwa wachezaji wote wa timu ya taifa ya nchi hiyo ambao wamefanikiwa kunyakuwa taji la Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka huko huko Niger Jumapili iliyopita. Katika hafla ya kuipokea timu hiyo katika ikulu, Keita amesema vijana hao wameionyesha dunia kuwa hakuna kusichowezekana kwa raia wa nchi hiyo. Rais huyo baadae alitangaza kumpatia kila mchezaji nyuma yenye thamani ya dola 24,000 na laptop zenye thamani ya dola 30,000. Kwa upande wa wachezaji waliokatisha masomo yao kwa ajili ya kwenda kuliwakilisha taifa lao watapewa darasa maalumu ili kufidia muda ambao hawakuwepo huku ofa ya kusomeshwa bure ikitolewa kwa wote ili kuwaruhusu kuendelea na masomo yao.

No comments:

Post a Comment