MENEJA wa klabu ya Sampdoria ya Italia, Sinisa Mihajlovic amempongeza Samuel Eto’o baada ya mshambuliaji huyo kufunga bao lake ya kwanza Serie A katika kipindi cha miaka minne wakati wa ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Cagliari. Eto’o alijiunga na timu hiyo kwa uhamisho huru Januari mwaka huu baada ya kuruhusiwa kuondoka Everton lakini alionekana kama angeweza kuondoka baada ya kuzozana na kocha kwa kukosa kufanya mazoezi. Hata hivyo, wawili hao walimaliza matatizo yao na sasa klabu hiyo inatumia faida ya kuwa na Eto’o kwa kupata ushindi huo muhimu jana. Akihojiwa Mihajlovic amesema anakipongeza kikosi chake kwa mchezaji mzuri na hususani Eto’o kwa kiwango bora alichokionyesha. Ushindi huo unaifanya Samdoria kukwea mpaka nafasi ya tano katika msimamo wa Serie A huku wakiwa wamebakisha alama tatu kufikia nafasi ya tatu katika msimamo ambayo itawafanya wafuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
No comments:
Post a Comment