TIMU ya Taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni inatarajiwa kucheza wa kirafiki na timu ya Taifa ya Misri kesho katika Ufukwe wa Escape One uliopo Msasani, Dar es Salaam. Akizungumza na wanahabari leo kuhusiana na mchezo huo, kocha msaidizi wa Tanzania Ali Sharif amesema pamoja na kipindi kifupi walichokuwa nacho toka timu ianzishwe lakini wamejiandaa vyema tayari kwa mchezo huo. Sharif amesema anajua kwa Tanzania mchezo huo bado ni mpya lakini anaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa mchezo huo utatoa fursa kwa vijana wa kitanzania kupata nafasi ya kujitangaza na kupata uzoefu kwani kwa nchi kama Misri wenyewe wameanza muda mrefu kucheza soka la ufukweni. Mchezo huo ambao utachezwa kuanzia saa 10 za jioni utakuwa hauna kiingilio kwa mashabiki ambao wangependa kushuhudia.
No comments:
Post a Comment