MSHAMBULIAJI wa Everton, Romelu Lukaku jana aliibuka shujaa kwa kuisaidia timu yake kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Dynamo Kiev ya Ukraine katika mchezo wa Europa League hatua ya timu 16 bora. Matokeo mengine ya mechi za mkondo wa kwanza zilizochezwa jana Villarreal ilishikisha adabu kwa kuchapwa mabao 3-1 na Wahispania wenzao Sevilla huku Zenit Saint Petersburg ya Urusi ikiiadhibu Torino ya Italia kwa mabao 2-0. Fiorentina wao walitoka sare ya bao 1-1 na AS Roma katika mchezo uliokutanisha timu zote kutoka Italia huku Waitaliano wengine Napoli wao wakiivurumisha Dynamo Moscow ya Urusi kwa mabao 3-1. Wengine walikuwa ni Wolfsburg ya Ujerumani ambao nao bila huruma waliiangamiza Inter Milan kwa mabao 3-1. Mechi za mkondo wa pili za michuano hiyo zinatarajiwa kuchezwa Alhamisi ya Machi 19 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment