KIUNGO wa Fiorentina, Milan Badelj amesema wamehuzunishwa baada ya kushindwa kulinda bao lao na kupelekea kutoka sare ya bao 1-1 na AS Roma katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Europa Leauge hatua ya timu 16 bora. Fiorentina walipata bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Josip Ilicic lakini Seydou Keita alisawazisha bao hilo zikiwa zimebaki dakika 13 baada ya Adem Ljajic kukosa penati. Badelj amesema walicheza vyema katika mchezo huo pamoja na kutoka kufungwa mabao 4-0 na Lazio. Kiungo huyo aliendelea kudai kuwa walipaswa kushinda mchezo huo lakini walijisahau na kujikuta wapinzani wao wakisawazisha huku wakikosa tena penati ambayo ingewapa ushindi.
No comments:
Post a Comment