Tuesday, March 24, 2015

HUWA SIPENDI KUWAKARIPIA WACHEZAJI WANGU - WENGER.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amekiri mara kadhaa kutaka kuwagombeza au kuwapigia kelele wachezaji wake lakini amekuwa mara nyingi amekuwa akijizuia. Arsenal bado imeendelea kujiimarisha katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu hivyo kuweka hai matumaini yao ya kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Akiulizwa mbinu anazotumia kuwasiliana na wachezaji wake, Wenger amesem mara nyingi huwa hapendi kuwa mkali au kuwapigia kelele wachezaji wake kwani hilo linaweza kuleta madhara zaidi. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa siku zote wakati timu inapofungwa hata wachezaji wenyewe hukasirika hivyo kama ukiendelea kuwakaripia badala ya kuongea nao taratibu unaweza kuwafanya wakapoteza hali yao ya kujiamini.

No comments:

Post a Comment