MSHAMBULIAJI wa klabu ya Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic anatarajiwa kukosa mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufungiwa mchezo mmoja kwa kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Chelsea. Mchezaji mwenzake Serge Aurier yeye amefungiwa mechi tatu kwa kumkosoa mwamuzi wa mchezo huo katika mitandao ya kijamii. Ibrahimovic alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi Bjorn Kuipers wa Uholanzi katika dakika ya 32 ya mchezo wao wa mkondo wa pili dhidi ya Chelsea kufuatia kumchezea faulo Oscar. Nyota huyo wa kimataifa wa Sweden, anaweza kukabiliwa na adhabu nyingine ya kufungiwa mechi nne kwa kauli aliyotoa kuhusu Ufaransa, mwishoni mwa mchezo wao dhidi ya Bordeaux.
No comments:
Post a Comment