MENEJA wa klabu ya Everton, Roberto Martinez amegoma kulaumu safu ya ulinzi baada ya kushuhudia kikosi chake kikichapwa mabao 5-2 na Dynamo Kiev ya Ukraine katika mchezo wa Europa League. Everton ambao waliingia katika mchezo huo wakiwa wanaongoza mabao 2-1 kutokana na ushindi waliopata katika mchezo wao wa awali, walijikuta wakitolewa kwa jumla ya mabao 6-4 baada ya makosa mawili ya kizembe katika kipindi cha kwanza kuwapata mabao muhimu dynamo. Akihojiwa Martinez amesema makosa machache yaliyofanywa na mabeki wake ndio yaliyowagharimu lakini pia alisifu jinsi kikosi chake kilivyocheza. Kutolewa kwa Everton kunamaanisha kuwa hakuna timu yeyote ya Uingereza katika michuano ya Ulaya.
No comments:
Post a Comment