Saturday, March 28, 2015

KOCHA WA UJERUMANI ADAI USHINDI KWAKE NI MUHIMU KULIKO MABAO.

KOCHA wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Loew amesema hatajali idadi ya mabao katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Georgia kwani jambo muhimu analotaka yeye na kushinda. Mabingwa hao wa dunia wamekuwa akisuasua toka washinde taji la Kombe la Dunia nchini Brazil baada ya kupoteza mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya mwakani dhidi ya Poland, sare ya nyumbani dhidi ya Ireland huku akiifunga Scotland kwa tabu. Jumatano iliyopita Ujerumani ilipata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Australia na sasa wanakabiliwa na kibarua kingine huko Tbilisi wakati Loew atakapokuwa akijaribu kusahau matokeo mabaya na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi dhidi ya Georgia. Ili kujiimarisha katika kundi lao la D. Loew amesema kwao hivi ushindi ndio jambo la muhimu na sio idadi mabao watakayofunga kwani wanahitaji alama tatu muhimu ili kujiimarisha katika kundi lao baada ya matokeo yasiyoridhisha katika michezo yao iliyopita.

No comments:

Post a Comment