Saturday, March 28, 2015

WELBECK AACHWA UINGEREZA KUTOKANA NA MAJERUHI.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Arsenal, Danny Welbeck ameondolewa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza baada ya kupata majeruhi ya goti katika mchezo dhidi wa kufuzu michuano ya Ulaya dhidi ya Lithuania jana ambapo walishinda kwa mabao 4-0. Majeruhi hayo ya Welbeck yalikuja kipindi cha pili cha mchezo huo ulifanyika katika Uwanja wa Wembley na kupelekea kutolewa nje katika dakika ya 77. Chama cha Soka cha Uingereza kilithibitisha majeruhi ya mchezaji na kudai kuwa tayri wameshamrudisha katika klabu yake kwa ajili ya vipimo zaidi. Welbeck sasa atakosa mchezo wa kirafiki wa kimataifa Jumanne ijayo dhidi ya Italia utakaochezwa jijini Turin.

No comments:

Post a Comment